Huwezi kusikiliza tena

Sheria ya mtandao yaanza Tanzania

Sheria ya Makosa ya mitandao inaanza kufanya kazi hii leo nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria hiyo yeyote atakayechapisha taarifa za uongo au zinazopotosha au ambazo hazijakamilika atakabiliwa na adhabu ikiwemo kifungo au kutozwa faini.

Sheria imekuja wakati ambapoTanzania inaelekea kwenye uchaguzi mkuu huku wadau wa habari wakidai kuwa ina nia ya kudhibiti utendaji wa wanahabari wakati wa uchaguzi

Prof Makame Mbarawa ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Technolojia amezungumza na Arnold Kayanda, kuhusu utekelezaji wa Sheria