Huwezi kusikiliza tena

Ntaganda kizimbani the Hague

Kiongozi wa waasi nchini Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo Bosco Ntaganda leo atafikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu huko the Hague.

Bosco Ntaganda aliongoza makundi kadhaa ya wapiganaji katika miaka ya tisini katika kile kilichojulikana kama vita vya pili vya Congo na aliendelea na harakati za uasi hata baada ya amri ya kukamatwa kwake.

Lizzy Masinga alizungumza na mwandishi wa mashariki mwa Congo, Byobe Malenga ambaye ameanza kueleza umuhimu wa kesi hiyo