Watu walioadhirika na pombe nchini Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Mamia waathiriwa na pombe Kenya

Uwanja wa michezo nchini Kenya umegeuzwa kuwa kituo cha muda cha kutibu maelfu ya watumiaji wa pombe na mihadarati. Juhudi hizi zinafanywa na Gavana wa Wilaya ya Murang'a, Mwangi wa Iria baada ya serikali kuchukua hatua kote nchini Kenya kufunga maeneo yanayotengeneza pombe haramu. Magazeti na vyombo vya habari huko Kenya yamekuwa na taarifa za maofisa wa tawala za mikoa wakipekua vilabu vya pombe na maficho ya ulevi kuwafurusha walevi na kuharibu bidhaa za kutengenezea pombe. Emmanuel Igunza ametuandalia taarifa ifuatayo.