Habre alazimishwa kwenda mahakamani
Huwezi kusikiliza tena

Habre alazimishwa kwenda mahakamani

Kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre inaendelea hii leo katika mji mkuu wa Senegal Dakar licha ya kiongozi huyo kukataa kuitambua mahakama hiyo.

Bwana Habre alilazimishwa kuingizwa mahakamani kwa nguvu alipokataa kuingia mwenyewe.

Kiongozi huyo alishikwa na walinzi alipomfokea hakimu pale upande wa mashtaka ulipoanza kusoma orodha ya majina ya watu waliouawa ama kupotea wakati wa utawala wake.

Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake mnamo miaka ya 80.

Pia anakabiliwa na mashtaka ya mateso na uhalifu dhidi ya ubinadamu,