Visa vya watu kijitia kitanzi vimeongezeka
Huwezi kusikiliza tena

Visa vya kujinyonga vyaongezeka Afrika

Shirika la afya ulimwenguni WHO, limesema kuwa visa vya matukio ya watu kujiua barani Afrika, inakaribia kuwa asilimia 11.4 ya visa vyote ulimwenguni kwa kila watu mia moja mwaka 2012.

Ikilinganishwa na mwaka wa 2000 na mwaka huo wa 2012, kuna ongezeko la asilimia 38 barani Afrika, hasa maeneo ya mashambani .

Visa vya watu kujiua vimezoeleka kuwa hutekelezwa na watu wazima, lakini kwa sasa vijana wengi hushirikisha na vitendo hivyo kwa kiasi kikubwa.

Regina Mziwanda amezungumza na Daktari Isaac Lema ambaye ni mtaalamu wa masuala ya magonjwa ya akili kutoka katika hospitali kuu ya Rufaa ya Taifa Muhimbili nchini Tanzania.