Mpango wa kuimarisha miradi ya kitafiti yaanzishwa Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Mpango wa miradi ya kitafiti waanzishwa Kenya

Mpango mpya wa kuziba pengo lililopo la kisayansi kati ya Afrika na mataifa yaliyoendelea umezinduliwa jijini Nairobi nchini Kenya. Mpango huo, unaojulikana kama AESA, umeanzishwa na wakfu wa Bill na Melinda Gates pamoja na Wellcome Trust. Tayari AESA wamepewa dola milioni sabini za kimarekani kufadhili miradi ya utafiti kama sehemu ya jitihada zake za kuimarisha uwezo wa kisayansi barani humo. Mwandishi wetu Anne Soy amechunguza upungufu wa sayansi barani na kuandaa ripoti hii.