Mwanamume mmoja raia wa Marekani amewastaajibisha wengi baada ya kuwasha moto kituo cha kuuzia mafuta ye petroli eti anachoma buibui.
Huwezi kusikiliza tena

Awasha moto kituo cha petroli kwa kuogopa buibui

Mwanamume mmoja raia wa Marekani amewastaajibisha wengi baada ya kuwasha moto kituo cha kuuzia mafuta ya petroli eti anaiangamiza buibui.

Yamkini buibui huyo ilikuwa ubavuni mwa gari lake.

Haijabainika kwanini aliamua kumchoma moto ilihali alikuwa katika kituo cha mafuta ya petroli.

Mafuta ya petroli huwaka kwa haraka sana.

Baadaye alikiri kuwa Hofu ya kuumwa na buibui huyo ilimzonga akajisahau na kuwasha kiberiti chake akiwa katika kituo cha petroli.

Kamera za siri katika kituo hicho cha Mobil kilichoko Van Dyke nje ya Center Line, Michigan.

Wengi waliotizama video hii wanamtaja kuwa ni mpumbavu,,,, je wewe ?

Toa maoni yako kupitia kwa ukurasa wetu wa Facebook na Twitter; tafuta BBCSwahili.