Jehovah Wanyonyi
Huwezi kusikiliza tena

Mtu aliyejiita 'mungu' nchini Kenya amekufa!

Je, wamkumbuka Jehova Wanyonyi Mkenya, kiongozi wa madhehebu wa kundi linalojiita Waisraeli waliopotea, ambaye mapema mwaka huu alisema kuwa yeye ndiye Mungu? Serikali ya Kenya imesema kuwa alifariki miezi mitatu iliyopita na wafuasi wake kuzika maiti yake mahali pasipo julikana. Hata hivyo wafuasi wake walisema kuwa Jehova Wanyonyi bado yu hai na anaendelea kufanyiwa matibabu katika hospitali moja nchini ingawa hawajui ni ipi.

Muliro Telewa alitembelea eneo alikotoka Jehova Wanyonyi katika kata ya Kipsomba magharibi mwa kenya na kutuandalia ripoti ifuatayo.