Huwezi kusikiliza tena

Haki za Binadamu Afrika, kusikilizwa?

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu itajadili suala la nchi za Afrika kuikubali mahakama hiyo ifanye kazi zake ipasavyo.

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu Jaji Augustino Ramadhan anatarajiwa kuongoza mjadala huo leo wa nchi za Afrika kukubali kusaini mkataba huo.

Aidha atakutana pia na wanasheria wa Afrika kusini kuishawishi nchi hiyo kutumia baadhi ya sheria zitakazowawezesha raia wake kuwasilisha malalamiko yao katika mahakama hiyo.

Sikiliza taarifa ya Omar Mutasa kutoka Afrika kusini, akieleza kwa kina.