Tatizo la maji bado sugu Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Tatizo la maji bado sugu Tanzania

Idhaa ya kiswahili ya BBC inaanza mfululizo wa makala ambazo zinamulika maisha ya kila siku na changamoto zinazomkabili Mtanzania hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Ahadi nyingi hutolewa wakati wa kampeni kuwapa moyo wapiga kura na matumaini kuwa maisha yao yataimarika pindi mtu, watu au chama fulani kinapochukua hatamu za uongozi.

Lakini kutokana na uzoefu wa wengi ahadi nyingi hazitimizwi, mfano ni tatizo la maji ambalo limeibuka kuwa sugu nchini Tanzania.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wanajua fika usumbufu unaosababishwa na ukosefu wa maji.

Tulanana Bohela amezungumza na wakazi hao.