Huwezi kusikiliza tena

Upinzani wadai kuchunguzwa Uganda

Taarifa kutoka nchini uganda, zinasema viongozi wa upinzani nchini humo wanamtuhumu rais Yoweri Museveni kwa kutumia mitambo maalumu ya kuwapeleleza ili kulinda maslahi yake binafsi na kuwazima katika mipango yao ya kumuondoa madarakani. Vifaa hivyo kutoka Uingereza vina uwezo wa kunasa maongezi ya simu ama barua pepe ya wapinzani hao na kupiga picha wakiwa sehemu mbali mbali nchini Uganda. Hii ni kwa mujibu wa nyaraka zilizoonekana kutoka kwa chombo cha uchunguzi cha kimataifa kiitwacho privacy international ambapo BBC ilipata kuzisoma baadhi ya nyaraka hizo.

Kulthum Maabad anasimulia