Kaimu mkurugenzi wa idara ya elimu ya wapiga kura Clarence Nanyari
Huwezi kusikiliza tena

Karatasi za kura zapelekwa vituoni Tanzania

Kaimu mkurugenzi katika idara ya elimu ya wapiga kura nchini Tanzania ameiambia BBC kwamba kutakuwa na zaidi ya vituo 60,000 vya kupigia kura katika uchaguzi wa mwaka huu.

Clarence Nanyaro vilevile amesema kuwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini humo, raia hawataruhusiwa kusalia eneo la mita 200 kutoka kituo cha kupiga kura baada ya kushiriki katika shughuli hiyo mbali na wapiga kura waliovalia sare zilizo na nembo za vyama vyao.