Je,uchumi wa Tanzania unatoa matumaini kwa raia wake.
Huwezi kusikiliza tena

Je,uchumi wa TZ unatoa matumaini kwa raia wake?

Suala la uchumi wakati wa uchaguzi ni nyeti. Watanzania wanaelekea kupiga kura Jumapili, bila shaka wanatathimini ni kiasi gani uchumi umegusa maisha yao mpaka sasa. Uchumi wa Tanzania unatajwa kutoa matumaini ya wengi kuingia katika kipato cha kati. Hata hivyo Benki ya Dunia inasema watu tisa kati ya kumi wanaingiza chini ya dola 3 kwa siku. Kwa maneno mengine, wengi hawajaguswa na ukuaji huu wa uchumi. Mwandishi wa BBC Sammy Awami amedodosa masuala kadhaa yanayohusu uchumi kujua hali halisi