Wasiwasi watanda Zanzibar kuhusu matokeo

Wasiwasi watanda Zanzibar kuhusu matokeo

Nchini Tanzania, maafisa wanaohusika na uchaguzi kwa siku ya pili wamekuwa wakihesabu kura.

Inasemekana uchaguzi huo umekuwa na ushindani mkali mno, ukilinganishwa na uchaguzi mwingine wowote ule uliowahi kufanyika nchini humo.

Mawaziri saba tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge, kulingana na matokeo yaliyopatikana kufikia sasa.

Tume ya uchaguzi inatazamiwa kutangaza matokeo kamili kufikia Alhamisi.

Lakini kisiwani Zanzibar, mgombea mkuu wa upinzani, tayari amejitangaza mshindi.

Sammy Awami anaelezea.