Mwanariadha
Huwezi kusikiliza tena

Mwanariadha aliyetumia njia ya mkato Marathon

Mwanamume mmoja nchini Kenya amegonga vichwa vya habari nchini humo kimataifa na pia kuwa mada kwenye mitandao ya kijamii baada yake kudaiwa kutumia njia ya mkato akitaka kudai ushindi mbio za Marathon.

Julius Njogu, 28, anadaiwa kujiunga na wanariadha mbio za Standard Chartered Marathon zikikaribia kumalizika. Mshindi wa mbio hizo za kilomita 42 huzawadiwa $7,000.

Maafisa walimshuku baada ya kugundua kwamba hakuonyesha dalili zozote za uchovu. Wanariadha walikuwa wakishindania uongozi pia walisema hawakumuona umbali wote waliokimbia.