Zanzibar
Huwezi kusikiliza tena

Mkuu wa tume Zanzibar ana mamlaka ya kufuta matokeo?

Baada ya uchaguzi wa amani visiwani Zanzibar, ghafla zilikuja taarifa za kushangazwa za kufutwa kwa matokeo. Katika tangazo lake, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Visiwani humo Jecha Salim Jecha alisema uamuzi wake umekuja baada ya kujiridhishwa kwamba uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba uligubikwa na mapungufu mengi.

Lakini uamuzi huo ulizua maswali mengi kuliko majibu. Mwandishi wa BBC Sammy Awami, ametafuta majibu ya maswali haya ya kisheria kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman.