Mercy Njoki
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke anayefaa wanaoishi mitaani Nairobi

Ni kawaida kwa watoto wa mitaani kusahauliwa na jamii na pia jamaa zao wakati wanapoondoka nyumbani, na kwa kawaida huishia kuwa kero katika jamii. Lakini mjini Nairobi, Mercy Njoki amejitolea kuwasaidia vijana hao maskini kupata mwamko mpya maishani.

Kando na kuwapa chakula na kuwasaidia vifaa vya kujinufaisha, Mercy husaidia vijana hawa kuungana na jamaa zao.

Anthony Irungu aliandamana na Mercy katika shughuli zake za kuwasaidia vijana hao na kutuandalia taarifa ifuatayo.