Maandamano ya kupinga muhula wa tatu nchini Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Je, unaichukuliaje hatua ya maraisi kujiongezea muda?

Kuna tabia moja ambayo inaonekana kutanda kote barani Afrika ambapo baadhi ya marais wamekuwa wakibadili katiba kuwapa muhula wa tatu.

Mfano mmoja wapo ni nchi ya Burundi ambayo baada ya Rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu sasa karibu kila uchao watu wamekuwa wakiuawa, huku upinzani ukikandamizwa na raia kutishwa. Kama ilivyotokea huko nchini Rwanda maelfu waliuawa nchini Burundi mwaka 1990 katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwandishi wa BBC alista leithiid (Alastair Leithead) ameandaa ripoti hii inayosimuliwa na David Wafula