Maalim Seif na Jakaya Mrisho Kikwete
Huwezi kusikiliza tena

Zanzibar:Yaliozungumzwa kati ya Kikwete na Seif

Rais wa Tanzania anayeondoka Jakaya Kikwete leo amekutana na kiongozi wa Upinzani visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad aliyedai kushinda katika uchaguzi mkuu uliopita na kuzungumzia hali ya kisiasa ilivyo visiwani humo, hususan baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jecha Salim Jecha kutangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25 mwezi Oktoba.

Halima Nyanza amezungumza na Mkurugenzi wa habari na Mawasiliano wa Chama cha Wananchi CUF Ismail Jussa ili kubaini kilichojaliwa katika mazungumzo hayo.