Shambulio la mjini Paris
Huwezi kusikiliza tena

Hivi ndivyo ilivyokuwa katika shambulio mjini Paris

Maafisa wa polisi walioijihami walivamia ukumbi moja wa muziki ili kumaliza utekaji uliotekelezwa na washambuliaji wakati wa shambulio la mji wa Paris ijumaa usiku.

Kundi moja la wasanii wa muziki wa roc lilikuwa likiwatumbuiza watu waliojaa katika ukumbi huo wenye viti 1500 wa Bataclan baada ya washambuliaji kuvamia na kuanza kuwafyatulia risasi raia.

Watu 80 wanadaiwa kufariki katika ukumbi huo.

Vikosi maalum vya usalama vilitumwa ili kuukabili uvamizi huo ,milipuko inasikika huku waliohudhuria tamasha hilo wakionekana kutoroka.