Huwezi kusikiliza tena

Watu zaidi ya bilioni 2 hawana vyoo

Takriban watu zaidi ya bilioni mbili Duniani hawana vyoo salama na vya kisasa,huku wengine wapatao bilioni moja hawana kabisa vyoo kwa mujibu wa ripoti ya umoja wa Mataifa, wanawake na watoto wanatajwa kuwa waathirika wakubwa wa ukjosefu wa vyoo.

Kutokana na hali hiyo Novemba 19 ya kila mwaka, Dunia huadhimisha siku ya choo duniani.

Mwandishi wa BBC David wafula alizuru mojawapo ya vitongoji duni jijini Nairobi na hapa anaanza kuzungumza na Bi.Zahra Hassan kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vyoo.