Taarab Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Ana kwa ana na mwana wa gwiji wa taarab Tz

Muziki wa Taarab, kama moja ya aina ya muziki ya Waswahili una historia ndefu. Tangu mwanzo wa karne ya ishirini Taarab imekuwa maarufu kisiwani Zanzibar, na Mwambao wa Afrika Mashariki kwa jumla. Mtindo wa kucheza ala kama vile oud, ganuni na violin pamoja na mashairi yake una muundo wake, ambao wapenzi na wasanii wa taarab wanaujua. Mmoja wao, Mohammed Issa Matona ambaye ni mtoto wa gwiji wa taarabu Issa Matona anacheza karibu ala zote zinazojumuishwa kwenye taarab.Mwanzo nimemwuliza anapenda ala gani zaidi.