Jawahir Musa
Huwezi kusikiliza tena

Chifu mwanamke anayeunganisha jamii Eastleigh

Jawahir Musa ni chifu katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi na kwa miaka kadhaa amekuwa kiunganishi kati ya serikali na wakazi wa mtaa huo.

Ingawa nafasi ya chifu wa kike huja na majukumu na changamoto tele, jinsia yake haijamzuia kuimarisha hali.

Licha ya Mtaa huo kupata umaarufu kwa vurugu na uvamizi wa mara kwa mara wa mabomu, Jawahir amechangiua kuimarisha usalama katika eneo hilo.