Fundi
Huwezi kusikiliza tena

Kituo chaanza kufunza kinadada ufundi

Fani za ufundi kama wa useremala, umeme, uungaji vyuma na nyinginezo nyingi zinafahamika na jamii kuwa ni kazi za wanaume.

Chuo cha ufundi cha Don Bosco nchini Tanzania kilikuwa kimejikita katika kutoa mafunzo ya ufundi kwa vijana wa kiume pekee, lakini hivi karibuni kimeamua kutoa mafunzo hayo kwa jinsia zote.

Chuo hicho pia kinakiendesha kampeni ijulikanayo kama binti thamani ili kuwahamasisha wasichana na jamii kwa ujumla kuwa kuna fursa nyingi ndani ya ufundi.

Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alitembelea kituo hicho na kuandaa taarifa hii.