Kerrow
Huwezi kusikiliza tena

Wanasiasa wa Mandera wahojiwa kuhusu makaburi

Wanasiasa watano kutoka eneo la Mandera, maskazini mashariki mwa Kenya waliokuwa wamekamatwa na polisi mapema hii leo, katika uwanja wa ndege wa Wilson mjini Nairobi, wameachiliwa huru.

Hii ni baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa katika makao makuu ya idara ya uchunguzi wa jinai kuhusu makaburi yaliyodaiwa kupatikana eneo la Mandera.

Mwandishi wa BBC Robert Kiptoo alizungumza na mmoja wao Seneta Billow Kerrow.