Ali Kiba
Huwezi kusikiliza tena

Ali Kiba asimulia maisha yake ya usanii

Ali Kiba ni miongoni mwa wasanii maarufu sana kutoka Tanzania ambaye amewika si nchini humo tu bali Afrika Mashariki na nje ya mipaka ya Afrika.

Msanii huyo ambaye amewahi kuimba na wasanii maarufu kama R Kelly na Neyo ametutembelea leo katika studio zetu hapa London.

Zuhura Yunus alizungumza naye mwanzo akitaka kujua kwanini alipotea kwa muda kwenye anga za muziki.