Rwanda
Huwezi kusikiliza tena

Mahakama ya mauaji ya Rwanda yafunga washukiwa

Mahakama Maalum ya Kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Jumatatu ilitoa hukumu yake ya mwisho, miaka 20 baada ya kuanza kazi.

Watuhumiwa sita walikutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya Kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. Mahakama hiyo, iliyokuwa na makao yake Arusha Tanzania, ilianzishwa kuendesha mashtaka ya watuhumiwa wakuu wa mauaji ya kimbari.

Watu tisini na mmoja walishtakiwa, na sitini na mmoja wakahukumiwa.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami anaripoti zaidi kutoka Arusha.