Huwezi kusikiliza tena

Wapiga kura Rwanda waamua

Raia wa Rwanda wamepiga kura ya maoni kufanyia marekebisho katiba itakayomruhusu Rais Paul Kagame kugombea Urais kwa awamu ya tatu.

Mabadiliko haya yatampa fursa ya kugombea na kuwa madarakani hadi mwaka 2034.

Ikiwa itapitishwa Rais atagombea tena mwaka 2017 awamu ya miaka saba na miaka mingine mitano kwa awamu mbili baada ya hapo.

Kwa mujibu wa serikali, karibu watu milioni nne tayari wamesaini makubaliano kumtaka Rais Kagame agombee tena.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Yves Buchana anaarifu zaidi.