Masanja
Huwezi kusikiliza tena

Masanja: Tutiwe moyo na kuzaliwa kwa Yesu

Masanja Mkandamizaji msanii wa maigizo kutoka nchini Tanzania ni miongoni mwa wachekeshaji waliofanikiwa kimaisha kutokana na uwezo wake wa kuwavunja mbavu, watazamaji na wasikilizaji.

Yeye hushiriki katika kipindi maarufu cha runingani cha Original Comedy.

Pamoja na umaarufu wake katika tasnia ya sanaa, Masanja pia ni mchungaji na mwimbaji wa nyimbo za injili.

Alizungumza na Esther Namuhisa kuhusu maana ya sikukuu ya Krismasi.