Kgatlhanye
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke atengenezaye mikoba ya wanafunzi

Thato Kgatlhanye ni mwanamke mjasiriamari kutoka Afrika Kusini ambaye kampuni yake hutengeneza mikoba maalum ya wanafunzi ya kubebea vitabu.

Mikoba hiyo imeundwa kwa kutumia mifuko ya plastiki ya kubebea bidhaa madukani.

Mikoba hiyo ina mitambo ya sola ambayo mchana hutega nishati ya jua ambayo hutumiwa usiku kutoa mwangaza na kusaidia wanafunzi kusoma.