Oromo
Huwezi kusikiliza tena

Waoromo waandamana Johannesburg

Raia wa Ethiopia wanaotokea katika jimbo la Oromo wameandamana hii leo katika makao makuu ya bunge la Afrika mjini Johannesburg wakitaka kilio chao cha kupigwa na kunyanyaswa na wakuu wa serikali ya Ethiopia kisikilizwe na viongozi wa Afrika.

Mwandishi wetu Omar Mutasa amezungumza na Yahya Abdulrahman mwanachama wa jamii ya Oromo wanaoishi nchini Afrika Kusini.