Kasa
Huwezi kusikiliza tena

Kasa abebeshwa kamera Kenya

Kampeni ya kuwarejesha watalii Pwani ya Kenya ilipata sura mpya baada shughuli ya kumwachilia kasa kurudi baharini kupeperushwa moja kwa moja kwenye mitandao eneo la Watamu.

Kasa wengi hunaswa kimakosa na wavuvi, na shirika moja linaendesha kituo cha kuwaokoa kasa hao na kisha kuwarejesha baharini.

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi alikuwa Watamu kushuhudia tukio hili, na kuandaa taarifa ifuatayo.