Ayot
Huwezi kusikiliza tena

Mke wa Dominic Ongwen azungumza

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ya ICC ya mjini The Hague, Uholanzi imeanza kusikiliza kikao cha kuamua iwapo kuna sababu ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Dominic Ongwen, mmoja wa makamanda wa kundi la waasi wa Uganda wa Lord Resistance Army, LRA.

Ongwen ambaye alijisalimisha kwa majeshi ya Marekani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati alifikishwa kwenye mahakama hiyo ili kujibu shutuma mbalimbali zikiwemo ubakaji, mauaji pamoja na makosa ya uhalifu wa kivita visa vilivyotekelezwa sehemu za kaskazini mwa Uganda pamoja na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mwandishi wetu Siraj Kalyango amekutana na mke wa Dominic Ongwen, Florence Ayot, mwenye umri wa miaka 36 pamoja na watoto kadhaa wa Ongwen.

Kwanza anamuelezea Dominic Ongwen.