Dominic Ongwen
Huwezi kusikiliza tena

Mahakama ya ICC yatathmini kesi ya Ongwen

Kamanda mmoja wa kundi la Lords Resistance Army, alifikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Domonic Ongwen alihudumu chini ya kiongozi wake Joseph Kony, mmoja wa washukiwa wanaosakwa zaidi duniani. Kikao hicho kilitathmini iwapo kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki. Baadhi wamehoji kwanini ashtakiwe mbali sana badala ya nyumbani Uganda. Siraj Kalyango amesafiri kijijini Lukode, kaskazini mwa Uganda ambako mauaji hayo yalifanyika mwaka 2004.