Nyoka
Huwezi kusikiliza tena

Uhaba wa dawa ya kuua sumu ya nyoka

Wataalamu wa matibabu wanaonya kwamba uhaba wa sumu ya nyoka huenda ikawa ni jambo ambalo litahatarisha maisha ya watu wengi barani Afrika.

Kusini mwa jangwa la sahara, zaidi ya watu milioni moja huumwa na nyoka kila mwaka, na wengine elfu thelathini hufariki dunia.

Tiba halisi ni kutumia dawa ambayo hutengenezwa kwa kutumia sumu ya nyoka.

Lakini sumu ya nyoka ni adimu, kama alivyogunuda Ferdinand Omondi, alipolitembelea shamba moja pwani ya Kenya.