Muliro
Huwezi kusikiliza tena

Maisha ya kifahari ya wanamuziki ni halisi?

Baadhi ya wanamuziki wa Afrika Mashariki na Kati wanajulikana kwa maisha yao ya hali ya juu, wanasema ni maisha ya bling bling.

Wasanii hawa ama kwa hakika wamekua ni mfano wa kuigwa na wanamuziki chipukizi wanaochipukia kwenye fani ya usanii. Lakini je, maisha wanayoishi ni halisi? Ama kwa wengine wanatuhadaa tu kwamba wako sawa.

Mwandishi wa BBC John Nene amezungumza na mwimbaji maarufu wa Kenya Gloria Muliro kuhusu swala hili huku akitutumbuiza na kibao chake Mpango wa Kando.