Huwezi kusikiliza tena

Zimbabwe yakumbwa na njaa

Takriban raia millioni 1.5 nchini humo wanakabiliwa na njaa, hii ni kulingana na ofisi ya shirka la umoja wa mataifa linalohusika na Chakula duniani, WFP kufuatia ripoti ya mwaka jana kuhusu mavuno duni yaliyotokana na ukame na elnino.

Zimbabwe imepokea mkopo wa dola milioni $200 kutoka benki ya African Export-Import ili kuiwezesha Kuingiza tani laki saba za mahindi.

Nchini Zimbabwe mashirika ya msaada, yanafanya kazi katika maeneo yaliyoathirka Zaidi.

Mwandishi wa BBC Taurai Maduna alisafiri hadi eneo la Hwange kaskazini magharibi mwa Zimbabwe na kutuandalia ripoti hii inayosimuliwa na David Wafula.