Mahiga
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yalalamikia India kuhusu wanafunzi

Serikali ya Tanzania imeilalamikia serikali ya India baada ya wanafunzi wanne Watanzania kushambuliwa na mmoja wao kuvuliwa nguo.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Dkt Augustine Mahiga ameambia Bunge la Tanzania kwamba serikali imetuma ujumbe wa kueleza kugadhabishwa kwake na yaliyowasibu wanafunzi hao.

Kadhalika, imeitaka India kuwatuma polisi kutoa ulinzi maeneo yote wanamoishi wanafunzi Watanzania.