Kasino
Huwezi kusikiliza tena

Msisimko wa uchezaji kamari Kenya

Huduma mpya za kucheza kamari nchini Kenya, zimevuma sana nchini humo, huku maelfu wakishirikia katika michezo ya kushinda mamilioni ya pesa kila wiki.

Huduma hizo za mtandao na simu za mkononi zilianza takriban miaka miwili iliyopita lakini sasa zimeshinda zile za awali zilizokuwa maarufu za kasino. Wadadisi wanasema michezo hiyo itaendelea kuimarika kutokana na idadi kubwa ya Wakenya ambao wanatumia simu za mkononi ambao ni zaidi ya milioni 36.

Aidha wataalama wa masuala ya kiuchumi wanasema katika miakamitatu ijayo, sekta hiyo ya kamari itakuwa za thamani ya zaidi ya dola milioni hamsini.

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza na mengi zaidi.