Museveni
Huwezi kusikiliza tena

Museveni anapanga kustaafu lini?

Ni siku ya mwisho ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Uganda. Wagombea wote wamekuwa katika harakati za mwisho mwisho kunadi sera zao na kuwashawishi wapiga kura. Rais Museveni ambaye anawania kwa muhula wa tano hii alikuwa jijini Jinja na vitongoji vyake Jumatatu. Uamuzi huu wake wa kugombea tena iliibua maswala mengi kuhusu umri wake, na kipindi kirefu cha utawala wake.

Zuhura Yunus alipata fursa ya kumwuliza maswali kadhaa katika kikao cha waandishi wa habari.