Laptop
Huwezi kusikiliza tena

Kuishi na mtoto mwenye ugonjwa wa autism

Tunaendelea na makala yetu ya afya ambapo wiki hii tunaangazia swala la akili na ustawi wake, misururu inayoendelea ya makala ya BBC, leo tunaangazia hali inayomkumba mtu ijulikanyo kama Autism.

Autism ni tatizo la kihisia linalotokea kwa watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na watu wengine. Watu wenye matatizo ya autism hawaonekani kama watu wa kawaida.

Muda mwingine hawapendi kuwaangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana na watu. Pia, hawapo vizuri katika kimawasiliano.

Mwandishi wetu David Wafula alitembelea familia ya Bw Maina Gatheru ambayo ina kijana anayekabiliwa na hali ya Autsim.