Huwezi kusikiliza tena

Mawakili Burundi waishtaki serikali ICC

Kundi la Mawakili wa familia kadha nchini Burundi limewasilisha mashtaka mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita mjini The Hague, Uholanzi na kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu visa vya mauaji ya kiholela nchini humo.

Mawakili hao wanataka maafisa wa Burundi wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za mauaji yalitokana na mgogoro wa kisiasa kufuatia hatua ya Rais Pierre Nkurunziza ya kuwania kwa muhula wa tatu.

Serikali ya Burundi imesema maafisa wake wako tayri kujitetea kuhusiana na tuhuma mbalimbali.

Kutoka Bujumbura, Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga anasimulia zaidi.