Stephen
Huwezi kusikiliza tena

Hatari ya kutokunywa maji ya kutosha Baringo

Je, unafahamu unywaji wa maji ni muhimu kwa afya yako? Asilimia sitini ya mwili wa binadamu ni maji na mtu hupoteza maji mwilini wakati unapokwenda haja ndogo au kutokwa na jasho.

Wataalamu wa afya wanashauri kuwa mtu anapaswa kunywa zaidi ya lita mbili ya maji kila siku kwa afya bora.

Lakini kwa wakazi maeneo ya Baringo na Marakwet nchini Kenya madaktari wamelalamikia kuongezeka kwa idadi ya watu wanoambukizwa ugonjwa wa uvimbe wa kibofu au cystitis kwa kimombo, unaosababishwa na ukosefu wa maji ya kutosha mwilini.

Mwandishi wetu Robert Kiptoo amezungumza na daktari Stephen Kurere.