Mahiga
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yakereka kunyimwa pesa za Marekani

Tanzania imehuzunishwa na hatua ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) kusitisha msaada wake wa awamu ya pili wa dola milioni 472.8 ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja pesa za Tanzania.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na hatua hiyo ya bodi ya MCC akisema "imepuuza hatua kubwa tu zilizopigwa kidemokrasia" nchini humo.