Wasafiri mashariki mwa DRC walalamikia maboya

Wasafiri mashariki mwa DRC walalamikia maboya

Wasafiri wanaotumia maboti pamoja na meli katika ziwa Tanganyika kwenye bandari ya Mushimbakye, tarafa ya Fizi, katika mkoa wa Kivu ya Kusini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanailaumu mamlaka ya safari za majini kwa kuzembea kuchukua hatua dhidi ya manahodha pamoja na waendesha maboti na meli, kutokana na ada za fulana za usalama zinazojulikana kama boya zinazopewa kila msafiri bandarini hapo.

Mwandishi wa BBC eneo hilo BYOBE MALENGA, alitembelea bandari hiyo ya Mshimbakye nakutuandalia taarifa hii.