Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yatakiwa kutotekeleza adhabu

Mahakama ya Afrika kuhusu haki za binadamu na watu, imeamuru serikali ya Tanzania kutotekeleza adhabu ya kifo kwa Bw Armand Guehi, raia wa Ivory Coast, kabla ya uamuzi juu ya rufaa aliyowasilisha mahakamani dhidi ya serikali ya Tanzania.

Guehi anaitihumu kukiuka haki zake za kimsingi wakati wa kesi yake kwenye mahakama za Tanzania.

Raia huyo wa Ivory Coast alikuhumiwa kifo nchini Tanzania baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake mwaka 2005.

Ifuatayo ni taarifa ya mwandishi wa habari aliyeko Arusha Bartazar Nduwayezu.