Panama
Huwezi kusikiliza tena

Ufichuzi wa nyaraka za Panama

Nyaraka milioni kumi moja za siri zimefichuliwa kutoka kwa moja ya kampuni zenye usiri wa hali ya juu duniani, kampuni ya Mossack Fonseca ya Panama.

Nyaraka hizo kwa jumla zimewataja viongozi 72 wa nchi wa sasa na wa zamani.

Gazeti la Sueddeutsche Zeitung, ndilo lililopata nyaraka hizo kwanza kisha likazikabidhi kwa chama cha wanahabari wapekuzi la International Consortium of Investigative Journalists. Kitengo cha BBC Panorama na gazeti la Uingereza la Guardian ni miongoni mwa mashirika 107 ya habari katika nchi 78 ambayo yamekuwa yakitathmini nyaraka hizo.

Kampuni ya Mossack Fonseca imesema imeendesha shughuli zake kwa miaka 40 bila kuvunja sheria.