Simba
Huwezi kusikiliza tena

Simba aingia shule ya upili Marekani

Polisi katika eneo la Granada Hills mjini Los Angeles katika jimbo la California walikabiliwa na kazi isiyo ya kawaida baada ya kulazimika kumdhibiti simba aliyekuwa ameingia katika shule moja ya upili.

Simba huyo alidungwa mshale wa kumtuliza na baadaye akarejeshwa porini.