Congo
Huwezi kusikiliza tena

Waliotimuliwa Brazzaville walalamikia hali Kinshasa

Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliofukuzwa mwaka 2014 nchini Congo Brazzaville, wanakabiliana na ugumu wa maisha na shida za kila namna katika kambi walimowekwa jijini Kinshasa.

Raia hawa wanalalamika kuwa wamesahauliwa na serikali yao na kudai kutupwa nje kwenye lindi la uchafu.

Mbelechi Msochi alitembelea kambi hiyo kujionea hali halisi.