Huwezi kusikiliza tena

Malkia Elizabeth aadhimisha miaka 90

Umati wa watu wenye heri njema, na wanasiasa kutoka vyama vyote vya kisiasa wamejitokeza kuungana na familia ya malkia wa Uingereza kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwake.

Katika kasri la Windsor nchini England bendi la jeshi lilipiga wimbo wa kumtakia siku ya furaha ya kuzaliwa malkia.

Watoto wa shule walimwimbia malkia wakati akiwasalimu na kuwashukuru kwa kufika huko kumpongeza.

Mizinga ya risasi ishirini na moja ilipigwa kama heshima kwa malkia anapoadhimisha miaka tisini.

Maelfu ya waingereza walijitokeza katika maeneo mengi nchini Uingereza kuadhimisha siku hiyo ya kuzaliwa kwake.

Odhiambo Joseph ametuandalia taarifa ifuatayo.